YANGA YAVULIWA UBINGWA, FAINALI SASA NI MBAO FC NA SIMBA SC


Yanga imevuliwa taji la Azam Federation Cup baada ya kufungwa 1-0 na Mbao FC ya Mwanza kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba.

Mbao FC sasa itamenyana na Simba ya Dar es Salaam katika mchezo wa fainali.

Bao pekee la Mbao FC lilifungwa dakika ya 27 mfungaji akiwa ni beki wa Yanga Andrew Vicent aliyejifunga wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa.

No comments