YANGA YAZIMA MPANGO WA AZAMA KUMNG'OA HAJI MWINYI NGWALI

YANGA amesikia mpango wa Azam kutaka kumsajili beki Haji Mwinyi Ngwali na sasa haraka ameitwa mezani na kupewa mchongo wa maana.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba taarifa za Mwinyi kutakiwa na Azam zimewafikia vigogo wa Yanga na haraka wanafanya mawasiliano na beki huyo wa kushoto na kumweka sawa.

Bosi mmoja alisema jukumu la kumaliza hatua ya kuwasainisha mikataba mipya wachezaji ambao wanamaliza, lipo chini ya Manji lakini vigogo wa Kamati ya mashindano wameshapewa kazi kuzungumza na mmoja baada ya mwingine na kuwapa mikataba ya awali wakianza na Mwinyi.

Katika kumaliza kazi hiyo Yanga imeshakamilisha yote na meneja wa  mchezaji huyo ambaye ni baba yake mzazi ambaye naye ameshakubali mwanae kubaki katika kikosi hicho.


“Tunafahamu kwamba Azam wanamtaka Mwinyi lakini huyu ni kijana wetu tumeshakubaliana nae karibu kila kitu tumeongea na baba yake kila kitu kipo sawa hakuna shida,” alisema momoja wa vigogo wa Kamati ya Utendaji.

No comments