ZAHIR ALLY ZORRO AIFAGILIA BONGOFLEVA… lakini asisitiza dansi ndio muziki wa kweli

MKONGWE wa dansi aliyepata kutesa na bendi za Kimulimuli na Mass Media, Zahir Ally Zorro ameifagilia bongofleva, licha ya kudai kuwa dansi ndio muziki wa kweli hapa Bongo.

Akiongea na Saluti5 nyumbani kwake Kigamboni, Zorro amesema kuwa, anavyoamini ni kwamba dansi ndio muziki “swadakta”, lakini hataacha kuimwagia sifa bongofleva kwani baadhi ya wasanii wake wanafanya kazi nzuri.

“Ndio maana hata mimi binafsi kuna baadhi ya wasanii nimekubali kushirikishwa nao katika vyimbo zao na zikafanya vizuri zaidi, hii ni kwasababu nawakubali hawa vijana ingawaje muziki wa kweli ni dansi,” amesema.


Akiichambua zaidi bongofleva, Zorro ambaye hivi sasa anajihusisha na muziki wa “mtu mmoja” katika hoteli za Lamada, jijini Dar es Salaam, amesema anauchukulia muziki huo kama ni kati ya “sanaa” tu kama ilivyo kwa ngoma za asili na nyinginezo.

No comments