2FACE AMTANGULIZA DEMU WAKE KWENYE MAFANIKIO ALIYOYAPATA

STAA wa muziki nchini Nigeria ambaye ametamba kwa muda mrefu, Innocent Idibia au “2 Face Idibia” amesema kuwa mafanikio yake kwa kiasi kikubwa yalichangiwa na mpenzi wake, Annie Idibia.

“Najua kila mwanaume atapenda kumsifia mke wake hata pale ambapo hastahili, lakini katika hili niwe muwazi, Annie amenifanya kuwa hivi nilivyo, alisema staa huyo.

“Hakuna hatua ambazo zimepita bila kuwa na mkono wake, kwangu ni mwanamke bora zaidi maishani,” aliongeza.

2 Face, nyota kutoka Nigeria alipata mafanikio makubwa baada ya kutoa kibao cha “You are My African Queen” ambacho kimekaa kwenye chati za muziki kwa muda mrefu.

No comments