Habari

AJAX ‘YABISHA’ HODI FAINALI EUROPA LEAGUE …yaibanjua Lyon 4-1

on

Ajax imepiga hatua kubwa ya kuinusa fainali ya Europa League baada ya kuichapa Lyon 4-1 katika nusu fainali ya kwanza iliyochezwa kwenye dimba la Amsterdam ArenA.
Nusu fainali nyingine itachezwa Alhamisi kati ya Celta Vigo na Manchester United.
Mchezaji wa Chelsea Bertrand Traore  anayekipiga kwa mkopo Ajax alitumia dakika 25 kabla ya kuandika bao la kwanza pale alipopiga mpira wa kichwa uliompita kipa  Antonio Lopes kabla Kasper Dolberg hajafunga la pili sekunde chache kuelekea mapumziko.
Dakika tatu baada ya mapumziko Amin Younes akafanya matokeo yawe 3-0 huku Mathieu Valbuena akiifungia Lyon bao pekee dakika ya 66.
Bertrand Traore akawa shujaa kwa kufunga bao la nne dakika ya 71.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *