ALICHOANDIKA LEO HAJI MANARA KUELEKEA MECHI YA YANGA NA MBEYA CITY

ALIYEKUWA msemaji wa Simba, Haji Manara ambae siku zote huwa haishiwi maneno ya shombo, leo ameshuka na kijembe kingine kwa watani zake, Yanga ambao jioni wataikabili Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika: “Kila la kheri wanaocheza leo teh the swali langu je, mtaendelea kutukimbiza au mmeshindwa??? Hii ni zaidi ya mbio za Marathon."

Kisha chini ya maneno hayo, Manara akaweka chati ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambayo inaonyesha kuwa Simba inaongoza Ligi ikiwa na pointi 29 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 27.

Manara kwa sasa amefungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka kokote nchini na kutakiwa vilevile kulipa faini ya sh. mil 9.   

No comments