Hatimaye ‘likizo/adhabu’ ya Ally Chocky imesitishwa na tayari mwimbaji huyo amerejea kazini kwenye bendi yake ya African Stars “Twanga Pepeta”.

Chocky alisimamishwa kwa miezi miwili kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kupewa muda ili amalize vimeo vyake (show) vya nje ya bendi.

Mwimbaji huyo angerejea kazini mwanzoni mwa mwezi Julai, lakini hatua hiyo imesitishwa na kuanzia wiki hii Chocky alishiriki maonyesho kadhaa ya Twanga Pepeta.

Jumamosi iliyopita mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka aliiambia Saluti5 kuwa tayari wamemalizana na Chocky na kwamba angerejea kazini kuanzia Jumatatu.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac