AMIS TAMBWE AGOMA KURUDI SIMBA SC... asema Yanga ndio klabu yake ya mwisho kuichezea Bongo

MSHAMBULIAJI Amisi Tambwe raia wa Burundi amefuta kabisa uwezekano wa kurudi Simba baada ya kusema kuwa hawezi kuchezea timu nyingine yoyote hapa nchini tofauti na Yanga ambayo ameifanya kuwa klabu yake ya mwisho.

Tambwe amesema kuwa hata kama mkataba wake utaisha kwenye kikosi cha Yanga atakuwa tayari kurejea kwao na sio kusaini tena kandarasi ya kuchezea Simba kwa mara nyingine.

“Tanzania ni sehemu nzuri kwangu lakini siwezi kukosa timu Burundi kama hapa itashindikana kuongeza mkataba mwingine.”

“Ni kweli mambo ya mpira huwa hayaeleweki lakini sioni ni kwa namna gani naweza kurudi Simba, hapana hilo kwa sasa haliwezekani nitamalizia mpira wangu Yanga,” aliongeza mshambuliaji huyo.

Amisi Tambwe tangu atue kwenye kikosi cha Yanga amekuwa mwiba mkali kwa mashabiki wa Simba kutokana na kuwafunga mara kwa mara pale timu hizo za watani wa jadi zinapokumbana kwenye michuano mbalimbali.

Mara ya mwisho alifunga bao lililokera zaidi kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuunawa mpira kwa mkono kabla ya kufunga bao, mbele ya Novatus Lufunga na David.    

No comments