AMISI TAMBWE AWATAHADHARISHA WAPINZANI MECHI ZIJAZO ZA LIGI KUU

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe amewaonya mabeki wa timu pinzani kwamba wasithubutu tena kuikamia timu hiyo hususan safu yao ya ushambuliaji na kwamba hiyo ni hatari kubwa kwao kutokana na ufundi walionao.

Tambwe alisema hayo dhidi ya mchezo wa Tanzania Prisons walioshinda mabao 2-0 ambapo alifunga bao la kuongoza kabla ya kumtengenezea Obrey Chirwa kwa kichwa kilifungwa pia kiasi kwamba mabeki wa Prison walifanya makosa kuwakamia ambapo hilo liliwachongea.

Mshambuliaji huyo raia wa Burundi alisema mabeki wamekuwa wakimkamia kwa kumkaba wakiwa wawili mpaka watatu kitu ambacho kimekuwa kikiwapa nafasi wenzake kusumbua na kujikuta mabeki hao wakijichanganya na kujikuta wakifungwa kirahisi kama ilivyowatokea Tanzania Prisons.

Mshambuliaji huyo alisema kocha wa timu hiyo George Lwandamina kwa mara nyingine alionyesha uwezo mkubwa katika mabadiliko yake mawili ambayo ndani ya dakika tano yakatengeneza mabao mawili ambayo ndiyo yalikamilisha ushindi huo ambao umewarudisha kileleni.

“Unajua mabeki hawa ni kama haw jitambui, angalia walivyo. Wametukamia kwa muda mrefu walikuwa wakinikaba mabeki wawili mpaka watatu lakini safu yetu ya ushambuliaji ni imara wakajikuta wanawapa nafasi wengine na baadaye kujisahau tukawafunga tu," alisema Tambwe.


“Mabadiliko ambayo kocha aliyafanya yalitupa uhai mkubwa ndio maana nasema huyu ni kocha hodari. Aliwaingiza watu ambao walikuwa na usuluhisho wa kutengeneza nafasi ndani ya dakika tano tukapata mabao hayo mawili, kwa sasa tunataka ubingwa hicho ndicho tunachozungumza sasa katika timu."

No comments