AMISI TAMBWE: NIMEPATA DAWA YA MABEKI WANAONIKAMIA KWENYE MECHI ZA LIGI KUU

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amisi Tambwe amesema kuwa amepata dawa ya mabeki wanaomkamia kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ambazo zinaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali.

Beki huyo alisema kwamba kuna wakati alikuwa akilazimika kutumia nguvu sana kwani baadhi ya timu hutumia mpaka mabeki watatu kumkaba mshambuliaji wanayemuhofia.

“Ligi ya hapa ni kama vita na hasa unapokumbana na timu za mikoani, zinapania sana na kuharibu ladha ya mchezo,” alisema Tambwe.

“Nimeshajua namna ya kucheza nao, nimekaa hapa kwa muda mrefu nikiwa kwenye kiwango cha juu, watu hapa wanatumia nguvu wakati wa kukaba.”


“Najua ni jinsi gani nitafanya ili niendelee kufunga mabao muhimu kwa ajili ya timu yangu, nataka kuhakikisha tunatetea ubingwa ili turudi kwenye michuano ya kimataifa mwakani.”

No comments