AMRI KIEMBA ASIFU UAMUZI WA HIMID MAO KWENDA KUFANYA MAJARIBIO ULAYA

KIUNGO wa zamani wa Azam FC, Amri Kiemba amesema kuwa uamuzi uliochukuliwa na Himid Mao Mkwami kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa Ulaya utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa siku za usoni.

Mkwami amekwenda nchini Denmark katika klabu ya Randers FC kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa ambapo atakuwa huko kwa siku 15.

“Ni jambo zuri kuona wachezaji wetu wanajaribu kutafuta fursa za kucheza soka Ulaya. Hii itakuwa na faida kubwa kwake na hata timu ya taifa itapata kitu kipya,” alisema Kiemba.

“Hapa panapumbaza sana akili za watu, maamuzi ya Himid kila mpenda michezo ya dhati lazima atayaunga mkono,” aliongeza.

“Ni fursa anayopaswa kuitumia vyema kwasababu huwa hazirudi mara mbili, unaweza tu kuona ni wachezaji wangapi wamekwenda wamerudi mikono mitupu, lazima tumuombee kwa faida ya taifa letu.”


Ikiwa Mao atafuzu hatua ya majaribio atakuwa ni mchezaji wa tatu kucheza Ulaya katika timu zinazoeleweka baada ya Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

No comments