ANDREW VINCENT "DANTE" AWASHANGAA WANAOMBEZA KWA KUJIFUNGA DHIDI YA MBAO FC


SENTAHAFU wa timu ya Yanga, Andrew Vincent “Dante” amewashangaa wanaobeza uwezo wake baada ya kujifunga kwa bahati mbaya kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza.

Dante amesema kuwa anawashangaa watu wanaomkejeli mitaani pasipo kujua kwamba mpira ni mchezo wa makosa na yeyote anaweza kukosea uwanjani hata kama ana jina kubwa kiasi gani.

“Yanga ndio klabu yangu wakati huu ambapo inanipa kula, nashangaa watu wanaonibeza kanakwamba nilipanga kuja uwanjani na kufanya makosa ya kizembe, ile ni sehemu ya mchezo tu,” amesema beki huyo.

“Popote duniani mpira ni mchezo wa makosa na hakuna mchezaji anayepanga kuvurunda mechi, sijui kwanini watu wanashindwa kuelewa hilo,” aliongeza beki huyo.

“Sijali sana yanayosemwa kwasababu hivi sasa akili yetu inatazama namna ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara na hilo linawezekana kwa jinsi tulivyojipanga.”


Mchezaji huyo alitua kwenye klabu ya Yanga akitokea Mtibwa Sugar ya mjini Morogoro na amekuwa moja kati ya nguzo muhimu za timu baada ya nahodha Nadir Haroub “Cannavaro” kukosekana uwanjani kwa muda mrefu sababu ya majeruhi. 

No comments