ARSENAL ILIVYOVUNJA MWIKO WA MANCHESTER UNITED NA MOURINHOUshindi wa bao 2-0 wa Arsenal dhidi ya Manchester United, umevunja mwiko wa United wa mechi 25 za mashindano yote bila kufungwa na kufanya mchuano wa ‘top four’ uzidi kunoga.

Aidha, ushindi huo pia unakuwa ni wa kwanza kwa Wenger dhidi ya Mourinho katika mechi 15 walizokutana.

Mabao ya Arsenal yaliwekwa kimiani na Granit Xhaka  dakika ya 54 na Danny Welbeck dakika ya 57.

Pamoja na kufungwa, lakini United imefanikiwa kuonyesha uwezo wa kipaji kipya kupitia kwa beki kinda Axel Tuanzebe aliyengara sana katika mchezo huo.

Arsenal (3-4-3): Cech 7; Holding 6, Koscielny (c) 6.5, Monreal 6.5; Oxlade-Chamberlain 7.5 (Bellerin 84), Ramsey 7, Xhaka 6.5 (Coquelin 76), Gibbs 7; Ozil 5.5, Welbeck 7 (Giroud 84), Sanchez 5


Manchester United (4-2-3-1): De Gea 6; Tuanzebe 6.5, Jones 6, Smalling 6, Darmian 6.5; Herrera 6.5 (Rashford 63, 6), Carrick 6; Mkhitaryan 5 (Lingard 60, 5), Mata 6 (McTominay 85), Rooney (c) 5.5;Martial 5

No comments