Habari

ARSENAL OUT TOP FOUR ..MAN CITY YA TATU, LIVERPOOL YA NNE, WATOTO WA MAN UNITED BALAA!

on

Arsenal imeibutua Everton 3-1 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya
England, lakini haijawasaidia lolote katika kusaka tiketi ya top four.
Matokeo hayo ya Arsenal yangekuwa na faida iwapo tu Liverpool
ingelazimishwa sare na Middlesbrough, lakini kinyume chake, Liverpool ikashinda
3-0 na kukamata nafasi ya nne.
Kwa mtaji huo, Arsenal sasa itacheza Europa League msimu ujao badala
ya Champions Legue ambayo kwa zaidi ya miaka 20 imekuwa ikishiriki mfululizo
ligi hiyo kubwa zaidi barani Ulaya kwa ngazi za vilabu.
Manchester City wameshika nafasi ya tatu baada ya kuinyuka Watford
5-0 lakini Crystal Palace ikashindwa kuzuia ‘muziki’ wa Manchester United
iliyojaza watoto wa timu B. United ikashinda 2-0.
Matokeo ya mechi zote za kufunga msimu wa Premier League ni kama
ifuatavyo:
Arsenal 3 – 1 Everton
Burnley 1 – 2 West Ham United
Chelsea 5 – 1 Sunderland
Hull City 1 – 7 Tottenham Hotspur
Leicester City 1 – 1 AFC Bournemouth
Liverpool 3 – 0 Middlesbrough
Manchester United 2 – 0 Crystal Palace
Southampton 0 – 1 Stoke City
Swansea City 2 – 1 West Bromwich Albion
Watford 0 – 5 Manchester City

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *