ARSENAL YAIREJESHA MANCHESTER UNITED NYUMBANI KWAKE


Arsenal imeitungua Southampton 2-0 kwenye mchezo wa kiporo cha Premier League na hivyo kupanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.

Kwa ushindi huo wa Arsenal, Manchester United ilikuwa nafasi ya tano imeshuka hadi nafasi ya sita ambayo kwa namna fulani inaonekana kama vile ndiyo maskani yake ya kudumu msimu huu.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 60 na Olivier Giroud dakika ya 83.

Southampton (4-2-3-1):  Forster 6; Soares 6, Stephens 6.5, Yoshida 6, Bertrand 6.5; Romeu 6.5, Davis 6.5; Ward-Prowse 6 (Boufal 70 min, 5), Tadic 5 (Rodriguez 80), Redmond 5.5 (Long 70, 5); Gabbiadini 6.5

Arsenal (3-4-2-1): Cech 6.5; Holding 6, Mustafi 6.5, Monreal 6; Oxlade-Chamberlain 6.5 (Bellerin 36, 6.5), Ramsey 6.5, Xhaka 6, Gibbs 6; Sanchez 7, Ozil 6 (Coquelin 89); Welbeck 5 (Giroud 80) 

No comments