ARSENAL YAUA 4-1 …utamu wa ligi wahamia ‘top four’


Baada ya Chelsea kutwaa ubingwa na huku ikionekana wazi kuwa Tottenham haipokonyeki nafasi ya pili, utamu wa ligi kuu ya England sasa umehamia kwenye vita vya kusaka nafasi mbili zilizobakia za ‘top four’.

Hali hiyo imewadia baada ya Arsenal kuishindilia Stoke City 4-1 na kujizatiti nafasi ya tano.

Manchester City, Liverpool, Arsenal na Manchester United zote zinagombea nafasi ya tatu na ya nne huku Tottenham ikihitaji pointi moja tu kwenye michezo yake mitatu iliyosalia ili kumaliza katika nafasi ya pili.

Mabao ya Arsenal yamewekwa wavuni na Olivier Giroud aliyefunga mara mbili, Mesut Oezil na Alexis Sanchez wakati bao pekee la Stoke City lilifungwa na Peter Crouch.

No comments