ASHA BARAKA NAYE AWACHANA WASANII WA DANSI WANAOKIMBILIA SINGELI


Mkurugenzi wa Aset inayomiliki Twanga Pepeta, Asha Baraka amewaponda wasanii wa dansi wanaohamishia nguvu zao kwenye muziki wa singeli.

Akiongea katika kipindi cha Weekend Bonanza cha Clouds FM Jumamosi usiku, Asha Baraka akasema muziki wa dansi unahitaji maboresho makubwa na anashangaa kuona wasanii wa dansi wanakimbilia singeli badala ya kuboresha muziki wao.

“Hebu waache kuwabana vijana wa watu, wamehangaika kutafuta muziki wao wa singeli, wasiende kuwabana huko, wakomae na muziki wao wa dansi,” alisema Asha Baraka.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo huku mwanamuziki wake Khalid Chokoraa ndiye kinara wa wasanii wa dansi waliojitosa pia kwenye muziki wa singeli.

No comments