BAADA YA FUNUNU ZA KASEKE KUTUA SIMBA, SASA NI NIYONZIMA NA NGOMA

TANGU juzi kumekuwa na habari kwamba mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke ametimiza dhamira yake ya kuitumikia Simba.

Kaseke alikuwa anawindwa na Simba kwa muda mrefu tangu akiwa Mbeya City na akasaini Yanga miaka miwili iliyopita, sasa anadaiwa kwamba ameshamaliza mkataba wake Yanga na ameamua kuhamia Simba.  

Kaseke ni mmoja wa wachezaji waliokuwa na mpango watatu waliokuwa na mpango wa kutua Simba.

“Mashabiki wa Yanga watashangaa kuona wachezaji wao wengine wawili wakiwa wanavaa jezi nyekundu na nyeupe. 

Inasemekana ni uamuzi wao ambapo inadaiwa wamekatishwa tamaa baada ya kusikia mwenyekiti wao, Yussuf Manji ameondoka Yanga,” amesema mmoja wa watu wa karibu na wachezaji hao.

Wakati Kaseke ameshatangaza kuondoka, habari zinasema kwamba, wachezaji wengine wanaoondoka Yanga ni kiungo wa kimataifa raia wa Rwanda, haruna Niyonzima pamoja na mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma.

Hata hivyo, kila mmoja anadaiwa kwenda katika timu tofauti. Wakati Ngoma anadaiwa kwenda Afrika Kusini, Niyonzima amekuwa akisema kwamba amepata dili nchini Malaysia.


Hata hivyo mashabiki wa Yanga wamekuwa wakilalamika kuwa wanajua wachezaji wote hao wanakwenda Simba.

No comments