BAADA YA KUITUNGUA YANGA SC, MBAO SASA YAJINASIBU KUIMALIZA SIMBA

YANGA  imefungwa na Mbao katika mchezo wa mwisho wa Ligi na hatua hiyo inaonekana itakuwa shubiri kali kwa Simba kuelekea mchezo wao wa fainali ya Kombe la FA.

Kushinda kwa mbao  Jumamosi kumeongeza mzuka katika kikosi hicho kuelekea mchezo huo wa fainali ambapo  sasa timu  hiyo ina uhakika wa kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Akizungumzia mchezo huo wa fainali, kocha wa Mbao, Ndayaragije amesema sasa  akili yao ni kucheza Kombe la Shirikisho na kwamba wanajipanga kuichapa Simba.

Ndayaragije amesema Simba wanafungika ambapo mchezo huo ungekuwa rahisi kwa wekundu hao endapo wangefungwa Jumamosi na kushushwa daraja, jambo  ambalo lingewapunguza nguvu wachezaji wake.

"Tumeshinda mchezo mgumu dhidi ya Yanga lakini pia sasa tumepata uhakika wa kubaki Ligi kuu msimu ujao, hii ni hatua muhimu kwetu,’’ alisema Ndayiragije.


"Tunajiandaa kucheza na  Simba, sasa sio timu ngumu. Tunataka kuhakikisha kwamba tulifungwa kimakosa katika mchezo wetu wa mwisho baina ya timu hizi, sasa wachezaji wangu wameongezeka morari kwa ushindi wa Jumamosi."

No comments