BAADA YA 'KUSIMAMISHWA' KAZI ALLY CHOCKY ATOA KAULI NZITO KUHUSU TWANGA PEPETA


Baada ya kudaiwa kusimamishwa kwa miezi miwili, mwimbaji Ally Chocky wa Twanga Pepeta, ameibuka na kauli nzito kuhusu bendi yake hiyo.

Chocky amesimamishwa hadi Julai 1 ingawa adhabu yake inaweza kupungua baada ya Twanga Pepeta kusema hawajamsimamisha bali wamempa muda ili amalizie vimeo vyake (show zake za nje ya bendi).

Wakati wengi wakitegemea kuibuka kwa bifu kubwa baina ya Chocky na wamiliki wa Twanga Pepeta, mwimbaji huyo amesema hana mpango wa kuondoka Twanga Pepeta.

Akiongea na Saluti5, Chocky alisema atautumikia mkataba wa mwaka mmoja uliobakia na hata baada ya hapo bado ataendelea kubaki Twanga Pepeta.

“Nadhani nilishakuambia zamani hii kauli na leo nairudia tena. Sina mpango wa kuondoka Twanga Pepeta, nitaitumikia hadi wenyewe waseme basi,” alisema Chocky.

No comments