BARAZA LA WAZEE LA SIMBA LAUPONGEZA UONGOZI WA KLABU SAKATA LA UDHAMINI WA SPORTPESA

WAKATI baadhi ya watu wakiulaumu uongozi wa klabu ya Simba kwa kile wanachosema kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya Sportpesa ya Kenya, wazee wa klabu hiyo wameupongeza uongozi wao chini ya rais Evans Aveva kwa kufanikiwa kupatikana kwa mkataba huo.

Mratibu wa baraza la wazee la Simba, Felix Mapua amekaririwa na mtandao mmoja wa michezo akisema kwamba wanawapongeza rais Aveva na wenzake kwa ubunifu huo.

“Inawezekana kuna sehemu wamekosea lakini inawezekana kurekebishwa lakini ukweli ni kwamba sisi tunawapongeza kwa kuwa mkataba huo unapunguza Simba kuendelea kuwa ombaomba,” amesema mzee huyo na kuongeza.

“Tunachfanya sisi ni kusihi uongoze uendelee kutafuta wadhamini wengine ili kuwa na uhakika wa fedha za uendeshaji wa klabu.”

“Simba iliingia mkataba wa miaka mitano na Sportpesa kutoka Kenya, ambao thamani yake ni sh. mil 888 kwa mwaka n ash. bil 4.9 kwa mwaka.


Lakini taarifa za uhakika ni kwamba Sportpesa wameiongezea Simba mkataba mpya wenye thamani y ash. mil 950 kwa mwaka na sh. bil 5.173 kwa miaka mitano.

No comments