BARCELONA NA REAL MADRID MWENDO MDUNDO, ZOTE ZAPIGA 4-1 …Neymar na Ronaldo usipime


Barcelona na Real Madrid zinaendelea kushikana pabaya kwenye mbio za kusaka taji la La Liga baada ya kila moja kushinda 4-1.

Wakati Real Madrid ikiinyuka Sevilla 4-1, Barcelona nao wakafanya hivyo hivyo kwa Las Palmas.

Cristiano Ronaldo akaifungia Real Madrid mara mbili huku Nacho Fernandez na Toni Kroos kila mmoja akifunga mara mmoja wakati lile la Sevilla likiwekwa kimiani na Stevan Jovetic.

Kwa upande wa Barcelona, Neymar alikuwa na siku njema kwa kufunga mabao matatu huku Luis Suarez akifunga mara moja. Bao pekee la Las Palmas lilifungwa na Pedro Bigas.

Barcelona inaongoza ligi kwa pointi 87  ikibakiwa na mchezo mmoja huku Real Madrid ambayo nayo ina pointi 87 inashika nafasi ya pili lakini ikiwa na faida ya mchezo mmoja mkononi.

No comments