BARCELONA YAZIDI KUPAA LA LIGA, MESSI APIGA 2 KATIKA USHINDI WA 4-1


Barcelona imezidi kupaa La Liga baada ya kuiangushia kichapo kikali Villarreal na kuvuna ushindi bao 4-1 huku Lionel Messi akifunga mara mbili.


Messi alifunga katika dakika ya 45 na 82 baada ya Neymar kufungua karamu ya magoli dakika ya 21 huku Luis Suarez naye akifunga dakika ya 64. Bao pekee la Villarreal lilifungwa na Cedric Bakambu dakika ya 32.

No comments