Habari

BEKI WA MBAO FC NAE ATOA ONYO KWA SIMBA MCHEZO WAO WA LEO

on

BEKI wa
timu ya Mbao FC, Yusuf Ndikumana amesema kuwa klabu ya Simba itarajie kukumbana
na kitu cha tofauti kwenye mchezo wao wa fainali ya Kombe la FA ambao
unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma baadae leo.

Yusuf alisema
kuwa wanatarajia Simba baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu bara akili yao
wamehamishia kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA ili wapate tiketi ya kwenda
kwenye Kombe la Shirikisho.
“Tunajua
namna walivyokamia mchezo huu kwa sababu ni kwa muda mrefu hawajapata nafasi ya
kushiriki michuano ya kimataifa ila wanapaswa kujua hata sisi tumejiandaa na
wala hautakuwa mchezo rahisi kwao.”
“Ni
kweli wana wachezaji wengi wenye uzoefu lakini mchezo wa fainali haujawahi kuwa rahisi, tumedhamiria kuwashangaza,” aliongeza.

Simba
inaingia uwanjani ikiwa imetoka kupishana na ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara
ambao umebebwa na Yanga kwa mara ya tatu mfululizo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *