BLACK FACE ASEMA ALIKUWA SAHIHI KUMBURUZA 2 FACE MAHAKAMANI KWA WIZI WA WIMBO

RAPA Black Face amesema kwamba alikuwa sahihi kumpeleka mahakamani 2 Face baada ya kuiba moja kati ya kazi zake.

Black face alimtuhumu 2 Face kwa kumuibia wimbo wake wa “Let Some Boy Love You” hali iliyosababisha ampeleke mahakamani.

Mastaa hao walikuwa pamoja kwenye kundi ambalo lilianzishwa mwaka 2000 na kuundwa na 2 Face, Innocent Idibia, Faze na Chibuzor Oji.

“Ndio, nipo sahihi kwa uamuzi wangu wa kumpeleka mahakamani kwa sababu ya wizi wa kazi yangu,” alisema staa huyo.

“2 Face na meneja wake walikula njama ya kuiba wimbo wa “Let Some Boy Love You” na kuamua kumshirikisha staa kutoka Marekani, Bridget Kelly.

No comments