BONDIA MAYWEATHER "USO KWA USO" NA 2FACE IDIBIA WA NIGERIA

BINGWA wa zamani wa ngumi za uzitowa juu duniani, Floyd Mayweather Jr raia wa Marekani, amepanga kukutana na mwanamuziki wa Nigeria, 2Face Idibia.

Rapa 2Facealithibitisha juu ya ujio huo kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kuwepo kwa tetesi za ziara hiyo.

“Bondia anayeishi kama rais atatua Nigeria Juni na atakuwa hapa kwa siku tatu,” ilisomeka sehemu ya taarifa iliyotumwa na 2Face.

Floyd amekuwa na mafanikio makubwa kupitia mchezo wa ngumi lakini analaumiwa kwa kuwa na matumizi mabovu ya hela.

No comments