BUTI LA YANGA LAMNUKIA MUSTAPHA BARTHEZ... Lwandamila haonyeshi kuwa na mpango nae

HALI ya kipa wa timu ya Yanga, Ally Mustapha “Barthez” imekuwa shakani baada ya mkataba wake kumalizika na haionekani kama mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wana mpango nae tena.

Kipa huyo amekuwa akisugua benchi kwa kipindi kirefu tangu mechi ya mzunguuko wa kwanza wa Ligi uliowakutanisha na timu ya Simba katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kuishia kwa mabao 1-1.

Simba walichomoa bao hilo dakika za lala salama kwa njia ya mpira wa kona iliyochongwa moja kwa moja na Shiza Kichuya na kutinga wavuni.

Tangu wakati huo kipa huyo hajapewa nafasi ya kusimamia lango katika michuano yote ambayo timu ya Yanga imeshiriki msimu huu.

Nafasi ya kipa huyo imekuwa ikishikiliwa na Benno Kakolanya aliyejiunga msimu uliopita akitokea kwenye klabu ya Tanzania Prisons ya jijini Mbeya.


Chanzo cha taarifa hii kinaeleza kuwa klabu ya Yanga ina mpango wa kumjumuisha katika wachezaji watakaopunguzwa msimu huu.

No comments