Habari

CESC FABREGAS AFIKISHA MIAKA 30 YA KUZALIWA KWAKE …hatma yake Chelsea bado kizunguzungu

on

Kiungo wa Chelesea Cesc Fabregas leo amegonga miaka 30 kamili tangu azaliwe, lakini bado nyota huyo wa Hispania hujui ni klabu gani ataitumikia msimu ujao.
Mkali huyo bingwa wa kusambaza pasi za uhakika, hana nafasi kwenye kikosi cha watu 11 kinachoanza chini ya Antonio Conte ingawa mara nyingi amekuwa mchezaji wa kwanza kuingia dimbani akitokea benchi huku akiambulia kuanza mara chache sana.
Licha ya kuwa mtu 12 kwenye kikosi cha Conte, lakini uwezo wake umezivutia Manchester United na Liverpool.
Ingwa duru za michezo zinasema Fabregas anataka kuihama Chelsea, lakini Manchester United na Liverpool si miongoni mwa chaguo lake.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *