CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU DAR CHAJIPANGA KUKABILI CHANGAMOTO

CHAMA cha mpira wa kikapu mkoa Dar es Salaam (BD), kimejipanga kuhakikisha wanafanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika mzunguuko wa kwanza na zitakazojitokeza katika mzunguuko wa pili utakaoanza hivi karibuni.

Akiongea na saluti5, mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa chama hicho, Haleluya Kavalambi amesema mzunguuko wa kwanza umekuwa na changamoto nyingi na mbalimbali.

Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kuingiliana na ratiba kwa baadhi ya timu kushiriki mashindano ya ndani na nje ya nchi na ukosefu wa viwanja kwa ajili ya kuendeshea Ligi hiyo.

“Hivi sasa chama kinajipanga kuhakikisha kuwa changamoto hizo hazijitokezi katika mzunguuko wa pili,” alisema Kavalambi.


Mkurugenzi huyo amesema kuwa sasa mchezo wa wanawake wa Jeshi Stars utafanyika mara baada ya kurudi nchini Kenya wanakoshiriki mashindano ya kimataifa.

No comments