CHELSEA SASA ISHINDWE YENYEWE …Tottenham yalambwa kimoja na West Ham


Ni sawa na kusema ngoma ya kitoto haikeshi. Tottenham imeweka rehani mbio zake za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kunyukwa 1-0 na West Ham.

Balaa kwa Tottenham lilikuja dakika ya 65 baada Manuel Lanzini kupachika wavuni bao pekee.

Kwa matokeo hayo, Chelsea sasa ina nafasi nzuri ya kutanua wigo wa pointi iwapo itashinda mechi yake ya Jumatatu dhidi Middlesbrough.


Chelsea inaongoza ligi kwa pointi 81 ikiwa imebakiza mechi tatu, huku Tottenham iliyobakiwa na mechi tatu inashika nafasi ya pili na pointi 77.

WEST HAM: Adrian 7; Fonte 7.5, Reid 8, Collins 7.5; Byram 7, Kouyate 6.5, Noble 7.5, Cresswell 8; Lanzini 8.5 (Fernandes 90), Ayew 7.5 (Snodgrass 84); Calleri 6.5 (Fletcher 89).

TOTTENHAM: Lloris 6, Walker 6.5 (Trippier 80 - 6), Alderweireld 5.5, Vertonghen 6 (Dembele 67 - 6), Davies 5.5, Dier 6.5, Wanyama 6.5 (Janssen 73 - 5.5), Son 5, Eriksen 6, Dele 5.5, Kane 6.

No comments