CHID BENZ ASEMA KALAPINA HAJUI KITU CHOCHOTE KUHUSU UNGA NA ATHARI ZAKE

RAPA Chid Benz ambaye ni muhanga wa matumizi ya dawa za kulevya, amesema kuwa pamoja na harakati anazozifanya kiongozi wa kundi la Kikosi cha Mizinga, Kalapina katika kupambana na vita hiyo, bado kuna mambo hayajui.  

Chid Benz amesema kuwa Pina anafanya vyema kwenye vita ya kupambana na dawa za kulevya lakini watumiaji ndio wenye uelewa mpana wa athari zake.

“Nimejifunza mambo mengi kuhusu athari za dawa za kulevya, nimekaa Rehab kwa miezi mitatu, sijawahi kukaa muda mrefu kama nilivyokaa wakati huu, najua mambo mengi,” alisema Chid.

“Pina anafanya vizuri lakini sidhani kama anajua kwa undani ni kwanini hasa inakuwa ngumu kwa vijana kuachana na unga na jinsi ambavyo wanajiingiza kwenye matumizi hayo,” aliongeza rapa huyo.


Chid Benz ni miongoni mwa wasanii walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya ambapo hivi karibuni alikuwa kwenye kituo cha elimu na dawa za kuondoa urahibu huo.

No comments