CHOCKY APIGA ‘BATA’ NA SWAHIBA WAKE NA KUSEMA MAISHA YANAENDELEA

Mwimbaji wa Twanga Pepeta Ally Chocky ambaye anaelekea kufupishiwa ‘likizo’ yake ya bila malipo, amesema maisha yanaendelea.

Jana jioni Chocky alikuwa kwenye moja ya migahawa ya kisasa Kinondoni sambamba na swahiba wake Sahad Said bin Mdoe na kusisitiza kuwa pamoja na yote yanayotokea kwenye kibarua chake, lakini bado yeye ni msanii wa Twanga Pepeta.

Mwimbaji huyo aliyeonekana kufurahia maisha kama vile hakuna kilichotokea ofisini kwake, akasema wakati mwingine unapaswa kukabiliana na changamoto zinazokukabili kwa vile hiyo ni sehemu ya maisha na hivyo maisha yanapaswa kuendelea.


Chocky alisimamishwa kwa miezi miwili kuitumikia Twanga Pepeta ili amalize kazi zake za nje ya bendi, lakini taarifa kutoka ndani ya Twanga, zinasema huenda mwimbaji huyo akarejea kazini wiki hii.
 Chocky akiwa na swahiba wake Sahad Said Mdoe
 Chocky na Sahad 


No comments