CHOKORAA, KALALA JR, CHOCKY, LUIZER KUKINUKISHA DODOMA NJE YA TWANGA MEI 27 …Msagasumu, Dullah Makabila ndani


Jumamosi ya Mei 27, patachimbika Dodoma pale wasanii nyota wa muziki wa dansi kutoka Twanga Pepeta watakapofanya onyesho la pamoja na wakali wa singeli.

Wasanii hao ni Khalid Chokoraa, Kalala Jr, Luizer Mbutu na Ally Chocky ambapo watabiga show ya kibabe sambamba na Msagasumu na Dullah Makabila.

Onyesho hilo ambalo limepewa jina la “Usiku wa Wababe” litafanyika ndani ya ukumbi wa Dodoma Carnival.

Hata hivyo wasanii hao wa Twanga Pepeta watashiriki onyesho hilo nje ya bendi yao. 

Waratibu wa onyesho hilo, Kalala Jr na Khalid Chokoraa wameiambia Saluti5 kuwa show hiyo pia ni maalum kwaajili ya mashabiki wa soka kujipongeza na kuliwazana baada ya fainali ya kombe la FA kati ya Simba na Mbao FC  itakayofanyika Dodoma  jioni  ya siku hiyo ya Jumamosi.

“Hatutakuwa na bendi yetu ya Twanga Pepeta, lakini tutakuwa na wanamuziki mbali mbali watakaotuwezesha kupiga live,” alisema Chokoraa.

No comments