CHRISTIAN BELLA ‘KUITEKA’ DAR LIVE JUMAMOSI HII


Mfalme wa masauti Christian Bella Jumamosi hii atakuwa na show matata ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala.

Mashabiki wa Mbagala na vitongoji vyake wanamsubiri kwa hamu kubwa Christian Bella baada ya kuadimika ukumbini hapo kwa takriban mwaka mzima.

Bella akiwa na bendi yake ya Malaika, atashuka na nyimbo mpya kabisa ukiwemo “Shuga Shuga” ambao bado haujasikika popote pale Dar es Salaam.

Mwimbaji huyo ambaye hivi karibuni alikuwa na ziara ndefu nje ya nchi, atasindikizwa na wadada wawili hatari kwa kushambulia jukwaa - Pam D na Gigy Money pamoja na wasanii wengine kibao.

No comments