DARASA AKIRI USHINDANI NI MKUBWA KWENYE MUZIKI HIVI SASA

NYOTA wa muziki wa Hiphop Bongo, Darasa amesema kuwa anaamini zaidi katika ushindani ambao upo sasa kwenye fani ya muziki tofauti na miaka ya nyuma.

Staa huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la “Hasara Roho” amesema kuwa hivi sasa wanalazimika kufanya kazi kwa bidii kwa kuhofia ushindani uliopo.

“Wasanii wanafanya vyema kwa sababu ya ugumu wa soko, hakuna mwanamuziki anayeweza kujilipia gharama za Studio kwa ajili ya kujifurahisha tu,” amesema Darasa.

“Fani imejaa misukosuko mingi sana, inabidi kutuliza akili sana ili kazi yakjo ipokelewe vyema na mashabiki kabla ya kuanza kupata shoo,” ameongeza.


Darasa amejipatia mafanikio makubwa kupittia kibao chake cha “Muziki” ukilinganisha na kazi zake zote alizowahi kuzifanya miaka ya nyuma.

No comments