DIAMOND AELEZA NAMNA ANAVYOOGOPA KURUDI KWENYE MAISHA YA "UGALI WA KULUMAGIA"

MSANII wa bongofleva, Diamond Platnumz amesemna kuwa woga wa kuporomoka kimaisha na kurudia maisha yake ya zamani kabla hajawa staa, ndio jambo pekee linalomfanya akomae kufanya kazi ya “kilo” kila uchao.

“Nimekua katika maisha ambayo sitamani tena kuyarudia, hata ndugu zangu na marafiki zangu wote wanajua hilo na ndio maana nimekuwa mwoga sana wa kurudi kule nilikotoka na sasa najibidiisha kufanya kazi nzuri ili niendelee kuwa huku niliko,” amesema Diamond.

Diamond amesema kuwa, wakati mwingine amekuwa mzito hata kupokea mashairi ya nyimbo kutoka kwa watu wanaotaka kumuuzia kutokana na kuona kuwa hazina uzito wowote ukilinganisha na zile ambazo anaziandika mwenyewe kwa kutulia.

“Mtu anakuletea mashairi unayaangalia unaona kabisa hayalingani na daraja langu na kwamba kama nitayafanyia kazi yanaweza kuniangusha hivyo naachana nae na kuamua kuumiza kichwa mwenyewe.”

No comments