DIAMOND PLATNUMZ KUKUTANA USO KWA USO NA CASSPER NYOVEST WA AFRIKA KUSINI

STAA anayeiwakilisha vyema Tanzania kwenye medani ya muziki, Diamond Platnumz anatarajia kukutana na rapa Cassper Nyovest wa Afrika Kusini kwenye shoo moja sambamba na Futurekutoka Marekani.

Future na Cassper watakutana Zambia kwa ajili ya kufanya shoo kabla ya kutua jijini Dar es Salaam.

Nyota wengine kutoka Marekani wanaotarajiwa kutua Afrika ni pamoja na Travis Scott na Bryson Tiller ambao watafanya shoo katika jiji la Johannesburg na Polokwane mwezi Juni, mwaka huu.


Itakuwa ni mara ya kwanza kwa rapa Future kufika Tanzania na Zambia na kufanya shoo ambapo mwaka 2016 alifika Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV Afrika Music Awards.

No comments