DIANA EDWARD ACHEKELEA UMISS TANZANIA NA KUSEMA UNAMPA MADILI MENGI

MREMBO wa taifa, Diana Edward ambaye alitwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2016, amesema kuwa shindano hilo limemfanya abande dili nyingi na kumwingizia fedha tofauti na alivyokuwa akifikiria kabla ya kujikita kwenye fani hiyo.

“Siwezi kuyabeza haya mashindano kwasababu yamepanua wigo wa majukumu yangu na kunifanya nipate kazi nyingi za kufanya kwa ajili ya taifa langu,” alisema mrembo huyo.

“Ukiwa mshindi katika mashindano haya unapata kazi nyingi za kufanya kwenye jamii zetu na hilo ndio jambo nililokuwa nikiliota kwenye maisha yangu.”


Mrembo huyo alishinda na kuwa Miss Tanzania kwenye mashindano yaliyofanyika jijini Mwanza mwaka jana lakini hata hivyo zawadi yake ya gari amekabidhiwa hivi karibuni.

No comments