DIDA WA TIMES FM AMTAKIA KHADIJA KOPA "HAPPY BIRTHDAY" NJEMA


MKALI wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani ndani Times Fm, mtangazaji Khadija Shaibu “Dida”, amempa salamu za pongezi kwa gwiji la kike la mipasho Bongo, Khadija Kopa kwa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo.

Akiongea katika kipindi chake hicho cha “Mitikisiko ya Pwani”, Dida amemwombea Kopa maisha marefu zaidi kwa Mungu, huku pia akimtaka aendelee kuwa na sauti nzuri ya kuvutia inayowapagawisha mashabiki wengi wa taarab.

“Ukimwangalia Kopa pamoja na utu uzima alionao, lakini bado anaonekana kama mtoto wa miaka 25 vile kwa sababu ya kujitunza na kujiheshimu, kitu ambacho wengi wamekuwa wakishindwa na kujikuta wakizeeka kabla ya wakati wao,” amesema Dida.

Kwa upande wake Kopa mwenyewe aliyeongea na saluti5 hivi punde, amesema kuwa anamshukuru Mwenyezi Mungu kuiona siku hii na kumuomba amuongezee umri mrefu zaidi.

No comments