DONALD NGOMA ATHIBITISHA KUONDOKA YANGA

DONALD Ngoma ambaye ni mshambuliaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, amethibitisha taarifa za kuondoka kwenye kikosi hicho.

Nyota huyo ambaye alikuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu baada ya kupata jeraha la goti, ameweka wazi mipango yake ya kuachana rasmi na Yanga katika kipindi hiki ambacho mkataba wake unamalizika
.
Taarifa zilizoifikia saluti5 kutoka kwa mtu wake wa karibu zinasema kuwa nyota huyo raia wa Zimbabwe amekaa mkao wa kutaka kuondoka Jangwani baada ya msimu kuisha.

“Ni kweli Ngoma ana mipango ya kuondoka Yanga, haonyeshi dalili yoyote ya kuendelea kubaki msimu ujao baada ya kukaa nje ya kikosi muda mrefu akiuguza goti,” kilisema chanzo cha taarifa hii.

Mshambuliaji huyo amekuwa kwenye wakati mgumu tangu kuanza kwa mzunguuko wa pili baada ya kupata jeraha ambalo lilisababisha aenguliwe kwenye mipango ya mwalimu katika kikosi cha kwanza.

Kuna tetesi kuwa mshambuliaji huyo amepata timu nchini Afrika Kusini alikoenda kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.

No comments