DONALD NGOMA KUPOKELEWA NA MKATABA MPYA YANGA

UONGOZI wa Yanga umethibitisha kwamba unajua kwa taarifa kwamba mshambuliaji wao Donald Ngoma yuko nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya mguu wake aliojitonesha.

Taarifa kutoka ndani ya Sekretarieti ya Yanga ni kwamba Ngoma aliuaga uongozi wa timu hiyo akitaka kwenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu ya kifundo cha mguu.

Bosi mmoja alisema kabla ya Ngoma kupewa ruhusa hiyo na katibu mkuu wao, Charles Mkwasa pia raia huyo wa Zimbabwe tayari alishapata baraka kutoka benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Geoge Lwandamina.

Alisema mshambuliaji huyo atarejea wakati wowote kuanzia wiki hii kuendelea na majukumu yake ambapo pia huenda akaingia moja kwa moja katika meza ya mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya.

“Uongozi una taarifa kuwa Ngoma hayupo nchini, aliuaga uongozi na kumpa ruhusa ya kwenda huko Afrika Kusini kufanya hayo matibabu ya mguu wake ambao umekuwa ukimsumbua sana,” alisema bosi huyo.

“Kuna muda maalumu amepewa wa matibabu hayo na kabla ya ruhusa yake kutolewa na katibu mkuu tayari alishapata baraka zote kutoka kwa benchi la ufundi tunamsubiri arudi tuanze naye mazungumzo ya mkataba mpya."

No comments