DONALD NGOMA MBIONI KUSAINI KANDARASI MPYA YANGA... aikana Simba na kusema hajawahi kuteta nao

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma amesema kwamba yupo mbioni kusaini mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo ili iwe sehemu ya fadhila ya kukaa nje ya kikosi kwa muda mrefu baada ya kupata jeraha la goti.

Mshambuliaji huyo mwenye nguvu amesema kuwa hajawahi kufanya mazungumzo na kiongozi yoyote wa Simba na wala hafikirii kujiunga na timu hiyo kama inavyoelezwa.

“Yanga ni timu iliyonipokea vizuri, bahati mbaya kwangu ni kwamba msimu huu sijaweza kucheza sana kwasababu ya matatizo ya kiafya, mpango wangu ni kuendelea kubaki hapa ili nilipe fadhila kwa klabu kunivumilia kwa kipindi kirefu,” alisema mshambuliaji huyo.

“Nina mapenzi na Yanga, ni sehemu nzuri niliyoizoea hivyo siwezi kusaini kwenye klabu nyingine tofauti na hii nchini Tanzania,” aliongeza nyota huyo.

Simba imekuwa ikihusishwa kutaka kumsajili Ngoma kwa kipindi kirefu tangu apate jeraha la goti na kukaa nje ya kikosi kwa muda mrefu msimu huu.


Ngoma alijiunga na Yanga msimu uliopita na kuisaidia kubeba ubingwa wa Ligi Kuu bara na Kombe la FA huku akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 24 katika mechi zote alizocheza.

No comments