EDDO SANGA KUIBUKA NA KIGONGO KIPYA "MOYO BAHARI" NDANI YA MSONDO NGOMA


EDDO Sanga (pichani kushoto) ambaye ni kati ya waimbaji mahiri wa Msondo Ngoma, anashuka na wimbo mpya ndani ya bendi hiyo, ambao ameupa  jina la “Moyo Bahari”.

Akiongea na saluti5, Eddo amesema kuwa muda si mrefu atakianzia mazoezi kibao hicho ambacho anadai, kama ilivyo kwa vibao vyake vingine vyote, nacho kitakuwa moto wa kuoteambali.

“Niko mbioni kukianzia mazoezi kibao hicho ambacho kimebeba ujumbe mzito kwa jamii kuhusiana na maisha tunayoishi,” amesema Eddo, kati ya watunzi hodari ndani ya Msondo Ngoma kwa sasa.

No comments