Manchester United itahitaji saa 24 zijazo kubaini iwapo itakuwa na  Eric Bailly na Luke Shaw kwenye mchezo wa wa kwanza wa nusu fainali ya Europa League dhidi ya Celta Vigo huku Hispania.

Mabeki hao wawili waliumia Jumapili katika mchezo wa Premier League dhidi ya Swansea na walifanyiwa vipimo Jumatatu. 

Kama nyota hao watashindwa kucheza dhidi ya Celta Vigo, basi Jose Mourinho atakuwa amewakosa wachezaji wake saba wa kikosi cha kwanza wakiwemo mabeki watano.


USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac