FAINALI NI REAL MADRID NA JUVENTUS …mbio za Atletico Madrid zaishia sakafuni


Real Madrid imeifuata Juventus kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuitoa Atletico Madrid kwa jumla ya bao 4-2.

Atletico Madrid iliyokuwa nyumbani ilipigana kufa na kupona kurejesha mabao 3-0 waliyofungwa kwenye mchezo wa kwanza lakini juhudi zao zikaishia kuvuna ushindi wa 2-1 ambao haukutosha kuwatupa nje Real Madrid.

Iliwachukua dakika 12 Atletico Madrid kufunga bao la kwanza kupitia kwa Saul Niguez na dakika nne baadae wakawaduwaza Real Madrid baada ya kufunga goli la pili lililokuja kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Antoine Griezmann.


Wakati mchezo ukiyoyoma kuelekea mapumziko Isco akatibua mipango ya Atletico kwa kuifungia Real Madrid bao pekee dakika ya 42. Real Madrid ndiyo mabingwa Watetezi.


No comments