FARID MUSSA MAMBO MAKUBWA HISPANIA

WINGA wa timu ya CD Tenerife ya nchini Hispania, Mtanzania Farid Mussa amemaliza vyema msimu wa Ligi akiwa na kikosi cha vijana kutokana na mchango wake wa mabao na idadi ya pasi.

“Nimeanza katika mazingira magumu sana kwasababu kwa muda mrefu sikufanya mazoezi na timu nilipokuwa Tanzania nikishughulikia suala langu la uhamisho lakini sasa naona mambo yameanza kujipa," alisema Farid.

“Ilikuwa ngumu kuonyesha uwezo wangu mwanzoni mpaka nilivyokuja timu ya taifa na kucheza mechi mbili dhidi ya Botswana na Burundi nilivyorudi Hispania nikabadilika kupitia maelezo,” alifsema Farid.

Farid aliongeza kuwa hivi sasa anasubiri uamuzi wa kocha wake wa vijana, Quico de Diego ili kumpandisha kwenye kikosi cha wachezaji wakubwa ambacho kipo chini ya Jose Luis Marti.


Farid aliondoka Azam na kujiunga na timu hiyo ya Hispania lakini suala lake lilikuwa na utata na kuibua gumzo kubwa nchini baada ya kuchukua muda mrefu.

No comments