FATHER MAUJI ASEMA KIFO CHA KANUMBA KIMEMPOTEZEA HAMU YA KUTAZAMA FILAMU ZA KIBONGO

MCHARAZAJI mahiri wa gitaa la Solo kutoka Yah TMK Modern Taarab, Mohammed Mauji amesema kwamba amepoteza msisimko wa kutazama filamu za Kibongo tangu kufariki kwa mkali wa Bongomuvi, Steven Kanumba.

Akiongea na saluti5, Mauji amesema kuwa, sababu kubwa ya kupotea kwa hamu ya kutazama sinema hizo ni namna ambavyo waigizaji wengi waliobaki wanavyokosa ubunifu tofauti na ilivyokuwa kwa Kanumba.

“Wakati wa kanumba, ingawaje pia alikuwa na makosa yake lakini afadhali kidogo kulikuwa na na unafuu tofauti na sasa ambapo waigizaji waliobaki wengi ni wauza sura tu,” amesema Mauji.


“Utakuta mwigizaji tangu aanze sanaa hajawahi kucheza uhusika wa mtu masikini, kila siku yeye ni tajiri tu, sasa utaona kwamba hiyo ni kitu ambayo haiwezekani katika sanaa.”

No comments