FEMI KUTI ALALAMIKIA SERIKALI YA NIGERIA KUHUSU TATIZO LA UMEME JIJINI LAGOS

FEMI Kuti, mtoto wa mwanamuziki maarufu nchini Nigeria, Fela Anikulapo Kuti amelalamikia serikali ya nchi hiyo kutokana na tatizo la muda mrefu la kukosa huduma ya umeme katika jiji la Lagos.

Kuti amesema kwamba katika eneo analoishi la Alagbole Akute kumekosekana huduma ya umeme kwa siku saba mfululizo.

“Tumekaa siku saba bila kuwepo huduma ya umeme katika jiji la Lagos,” alisema mwanamuziki huyo.

Mwanamuziki huyo wa miondoko ya Afrobeat alisema hayo wakati alipokuwa kwenye shoo yake ya New Afrika Shrine.  


No comments