FUNKE AKINDELE APANGA KUINUA VIPAJI VYA CHIPUKIZI WA FILAMU NIGERIA

STAA wa filamu na maigizo nchini Nigeria, Funke Akindele amesema kuwa ana mpango wa kuanza kuinua vijana wanaochipukia kwenye kazi ya sanaa nchini humo.

Funke alidai kuwa anafahamu ugumu wanaokumbana nao wakati wanatafuta jinsi kufanikiwa kupitia sanaa.

“Sio kazi rahisi kufika juu, hata mimi nilitumia nguvu kubwa wakati naanza uigizaji. Kuna vikwazo vingi kuanzia ngazi ya familia mpaka kwenye Studio za kutengenezea filamu,” alisema.


“Napanga kuja na mpango wa kuanza kuwainua wasanii wachanga, nadhani natakiwa kurudi nyuma na kuwasaidia wale walio chini,” aliongeza.

No comments