GARETH BALE ATETA NA MANCHESTER UNITED ...SAFARI YA OLD TRAFFORD YANUKIA

Manchester United imeripotiwa kuwa mazungumzoni na Gareth Bale ili atue Old Trafford msimu ujao.
Winga huyo wa Real Madrid anadaiwa kuvutiwa na Manchester United lakini ni mpaka kikosi hicho cha Jose Mourinho kiwe na tiketi ya kucheza Champions League.
Gazeti la Hispania Diario Gol linaandika kuwa Real Madrid ipo tayari kumuuza Bale iwapo ofa sahihi itawekwa mezani.
Bale anatajwa kuwa na makubaliano ya mdomo na Mourinho kuwa atajiunga na Manchester United pindi atakapoamua kurejea Premier League.
Rekodi ya majeruhi ya mara kwa mara ya Bale inamfanya rais wa Real Madrid, Florentino Perez aangalie uwezekano wa kumpiga bei.
Bale mwenyewe ameweka wazi kuwa ni timu nne tu zinazoweza kumfanya ang'oke Real Madrid nazo ni Manchester United, Chelsea, PSG na Bayern Munich.

No comments